Ameota kuwa ni katika watu wa Peponi

Swali: Mwenye kuota kwamba ni miongoni mwa watu wa Peponi ahukumiwe kuwa ni katika watu wa Peponi?

Jibu: Hashuhudiwi Pepo isipokuwa yule aliyeshuhudiwa na maandiko. Haifai kwa njia ya kuota. Ndoto haizingatiwi. Lakini ndoto inaweza kuwa kweli ikiwa inatokana na mtu mwema:

“Ndoto nzuri anayoiona muumini au mwengine akaiona kwa ajili yake.”

Ni miongoni mwa bishara njema. Ama kuhukumu kwayo au kuitendea kazi haifai. Haifai kutendea kazi mambo ya ndoto.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://shrajhi.com.sa/fatawa/51/%D9%87%D9%84-%D9%8A%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A8%D8%A7%D9%84%D8%AC%D9%86%D8%A9-%D9%84%D9%85%D9%86-%D8%B1%D8%A4%D9%8A-%D9%81%D9%8A-%D8%A7%D9%84%D9%85%D9%86%D8%A7%D9%85-%D8%A3%D9%86%D9%87-%D9%85%D9%86-%D8%A3%D9%87%D9%84%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 03/01/2020