Ameona jua baada ya ndege kuruka juu


Swali: Mtu ambaye jua limemzamia na muadhini ameadhini akiwa kwenye uwanja wa ndege ambapo akakata swawm na baada ya ndege kuruka akaliona jua. Je, ajizuie?

Jibu: Jibu langu juu ya hili ni kwamba si lazima kujizuia. Kwa sababu uliwaingilia wakati wa kukata funga wakiwa chini ardhini na jua lilikuwa limekwishazama ilihali wako sehemu ambayo jua limekwishazama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukielekea huko na mchana ukaelekea kule na jua likazama, basi amekwishafugua aliyefunga.”[1]

Kama alifutari ambaye jua limemzamia akiwa kwenye uwanja wa ndege siku yake imekwisha. Siku yake ikishakwisha basi haimlazimi yeye tena kujizuia isipokuwa katika siku ya pili. Kujengea juu ya hili si lazima kujizuia katika hali kama hii. Kwa sababu kufungua kulikuwa ni kwa muqtadha wa dalili ya Kishari´ah. Hivyo si lazima kujizuia isipokuwa kwa muqtadha wa dalili ya Kishari´ah.

[1] al-Bukhaariy (1941).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Arkaan-il-Islaam, uk. 283
  • Imechapishwa: 15/05/2019