Amenuia kufunga Sha´baan kisha akaumwa


Swali: Kuna mtu amenuia kufunga Sha´baan. Katikati ya masiku ya Sha´baan akagonjweka ambapo akaacha kufunga. Mwishoni mwa Sha´baan akafunga. Je, anapata thawabu kwa yale masiku aliyonuia?

Jibu: Kunatarajiwa kwake kupata thawabu kwa yale aliyonuia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mja anaposhikwa na ugonjwa au akasafiri, basi anaandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akifanya katika kipindi cha afya yake.”

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika kila kitendo kinategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa kile alichonuia.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alifta.net/Fatawa/fatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=8&PageNo=1&BookID=12
  • Imechapishwa: 18/04/2018