Inafaa kumpa masikini mmoja kiwango cha kafara ya watu wawili?

Swali: Kuna mtu alimwingilia mke wake mchana wa Ramadhaan siku mbili mfululizo. Anakuwa analazimika kutoka kafara mbili juu ya siku mbili. Mtu huyu anatakiwa kuwalisha masikini 120. Je, inajuzu kwake kuwalisha masikini 60 badala ya masikini 120 kwa njia ya kwamba anampa kila mmoja kiwango cha watu wawili au ni lazima ampe kila mmoja kiwango chake na hivyo awe amewalisha masikini 120?

Jibu: Ni wajibu kwa yule aliyefanya jimaa mchana wa Ramadhaan atubu, aombe msamaha na kulipa yale masiku aliyofanya jimaa pamoja na kutoa kafara kwa kila siku moja. Kafara ni kuacha mtumwa huru. Asipoweza afunge miezi miwili mfululizo. Asipoweza alishe masikini sitini. Hakuna kipingamizi kutoa kafara mbili au zaidi kwa masikini sitini.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/326)
  • Imechapishwa: 18/06/2017