Swali: Tulisafiri kwenda katika likizo na tukamwacha kuku kwenye jumba lake na tukamwekea chakula na maji vya kumtosheleza. Lakini baada ya kurudi kwetu tukamkuta amekufa pamoja na kuzingatia kwamba tulikuwa na yakini kuwa yale maji yatamtosha. Kipi kinachotulazimu juu ya hilo?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hamkuzembea. Mlimwekea maji na chakula ambapo akafa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Aliingia Motoni mwanamke kwa sababu ya paka aliyemfungia ndani hadi akafa; hakumlisha wala hakumwacha aende kutafuta chakula kwa kula vijidudu vya ardhini.”

Huenda mtu akasema kwamba kuna uwezekano alikufa kwa sababu ya joto. Tunasema kwamba joto ni kitu kisichojulikana mpaka tuseme kuwa ulizembea kwa kutokufanya hatua dhidi yake. Midhali mahali hapo alipokuwepo kuku huyo ni penye kivuli cha kawaida, basi huna juu yako dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (57) http://binothaimeen.net/content/1309
  • Imechapishwa: 26/10/2019