Ameapa kutoswali kwenye msikiti fulani

Swali 395: Kuna mtu aligombana na mwenzake msikitini kisha akaapa kwa talaka kwamba hatoswali msikitini halafu akajuta. Afanye nini?

Jibu: Talaka inahesabika kwake ikiwa amenuia talaka kutokana na Hadiyth isemayo:

“Hakika kila kitendo kinategemea nia.”

Akinuia kisha akajutia na hapo kabla alikuwa hajamtaliki talaka mbili, basi talaka inahesabika kwake. Vinginevyo aende kwenye msikiti mwingine na hana ulazima wa kuswali katika msikiti maalum miongoni mwa misikiti. Ana haki ya kwenda kwenye msikiti mwingine.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 664
  • Imechapishwa: 14/12/2019