Ameahidi kusoma kurasa kadhaa kila siku


Swali: Mimi ni kijana ambaye nimemuahidi Allaah kusoma ufupisho wa tafsiri ya Ibn Kathiyr kurasa kadhaa kwa siku. Lakini hata hivyo sijatekeleza ahadi hii. Pamoja na kuzingatia kwamba nimejipangia muda huu na umemalizika. Je, kipi kinachonilazimu?

Jibu: Ni lazima kwako ujitahidi katika hilo. Ukifikwa na mapungufu katika baadhi ya siku basi ni lazima kwako kutubu kwa Allaah kutokamana na hilo. Huna kafara muda wa kuwa hukuapa. Ama ikiwa ahadi hii iliambatana na tamko kama mfano wa kusema (والله), (وتالله) na (وبالله) basi ni lazima kwako kutoa kafara ya kiapo. Amesema (Subhaanah):

لَا يُؤَاخِذُكُمُ اللَّـهُ بِاللَّغْوِ فِي أَيْمَانِكُمْ وَلَـٰكِن يُؤَاخِذُكُم بِمَا عَقَّدتُّمُ الْأَيْمَانَ ۖ فَكَفَّارَتُهُ إِطْعَامُ عَشَرَةِ مَسَاكِينَ مِنْ أَوْسَطِ مَا تُطْعِمُونَ أَهْلِيكُمْ أَوْ كِسْوَتُهُمْ أَوْ تَحْرِيرُ رَقَبَةٍ ۖ فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ ثَلَاثَةِ أَيَّامٍ ۚ ذَٰلِكَ كَفَّارَةُ أَيْمَانِكُمْ إِذَا حَلَفْتُمْ ۚ وَاحْفَظُوا أَيْمَانَكُمْ ۚ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ

“Allaah hatokuchukulieni kwa viapo vyenu vya upuuzi, lakini atakuchukulieni kwa viapo mlivyoapa kwa nia mlioifunga imara. Hivyo basi, kafara yake ni kulisha maskini kumi chakula cha katikati mnachowalisha familia zenu, au kuwavisha nguo, au kuacha huru mtumwa. Lakini asiyeweza kupata, basi afunge siku tatu. Hiyo ndio kafara ya viapo vyenu mnapoapa – na chungeni viapo vyenu. Hivyo ndivyo Allaah anavokubainishieni Aayah Zake ili mpate kushukuru.”[1]

[1] 05:89

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (09/389)
  • Imechapishwa: 29/07/2021