Ambaye wakati fulani anapotelewa fahamu ni wajibu kufunga?

Swali: Kuna mtu ambaye wakati mwingine anapoteza fahamu masaa kadhaa. Je, ni wajibu kwake kufunga?

Jibu: Akiwa ni mwenye akili na anapoteza fahamu baadhi tu ya masaa, basi ni wajibu kwake kufunga. Ni kama mfano wa yule ambaye analala baadhi ya nyakati. Kile kitendo chake cha yeye kupotelewa na fahamu baadhi ya nyakati katikati ya mchana au katikati ya usiku hakumzuilii kwake kufunga. Tunamuombea kwa Allaah amponye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/210 )
  • Imechapishwa: 24/05/2018