Alama kubwa za Qiyaamah kwa mpangilio

Swali: Je, mtu anaweza kuzipangilia alama kubwa za Qiyaamah?

Jibu: Kuna alama nne zilizo kwa mpangilio; al-Mahdiy, kisha atafuatia ad-Dajjaal, kisha kuteremka kwa ´Iysaa, halafu Ya´juuj na Ma´juuj. Ama kuhusu zilizobaki hazitokuja kwa mpangilio: moshi utaoenea ardhini, kuvunjwa kwa Ka´bah, kunyakuliwa Qur-aan kutoka kwenye misahafu na kutoka kwenye vifua. Alama za mwisho ni jua kuchomoza kutoka magharibi, mnyama atayetoka, kisha moto utaotoka upande wa Aden ambao utawafukuza watu na kuwaelekeza kwenye uwanja wa hesabu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 07/08/2018