al-Qaradhwaawiy na vifaranga vyake mtazamo wao juu ya Jihaad

Swali: al-Qardhwaawiy anasema kuhusiana na Jihaad:

“Kuhusina na suala hili maoni yangu ni yale yale kama ya wanachuoni wa waislamu wa leo Shaykh Raashid Ridhwaa´, Shaykh Shaltuut, Shaykh ´Abdullaah Daraaz, Shaykh Abu Zahrah na Shaykh al-Ghazaaliy. Wote hawa wanamaanisha kuwa Jihaad katika Uislamu iko kwa ajili ya kutetea Uislamu, nchi, utukufu, ardhi na heshima. Jihaad haikuwekwa kwa ajili ya kushambulia ulimwengu mzima, kama wanavyofikiria baadhi ya watu.” al-Islaam wal-Gharb, uk. 19.

Je, ni kweli kwamba Jihaad katika Uislamu imewekwa kwa lengo tu la kujitetea? Je, hawa waliotajwa ndio wanachuoni wa waislamu?

Jibu: Tumemraddi Raashid Ridhwaa´ kwa kitabu chenye kichwa cha khabari “Ruduud Ahl-il-´Ilm”. Himdi zote ni za Allaah kuona vilevile ameraddiwa na wengine, lakini hakuna aliyemraddi vizuri kama nilivyofanya kutokana na ninavyojua. Nampa changamoto kila yule mwenye kusema kuwa ni Salafiy anitajie mwanachuoni yeyote wa ki-Salafiy anayesema kuwa ad-Dajjaal ni picha ya ndoto. Hivyo ndivyo alivyomnukuu mwalimu wake mmisri Muhammad ´Abduh katika “Tafsiyr-ul-Manaar”. Baada ya hapo akakubaliana naye na wala hakumkosoa. Anapinga vilevile jua kuchomoza kutoka magharibi. Anasema kuwa hakuna kipingamizi chochote kinachosema mwanaadamu kuwa na baba mwingine mbali na Aadam. Haya yanasemwa na Muhammad ´Abduh. Raashid Ridhwaa´ ameyanukuu katiika “Tafsiyr-ul-Manaar” kwa njia ya kuyakubali. Ni upotevu wa wazi.

Kuhusu Shaltuut, kuna ndugu mmoja anayeitwa ´Abdullaah al-Yaabis ambaye kaandika kitabu chenye jina ”I´laam-ul-Anaam bi Mukhaalafaati Shaykh-il-Azhar Shaltuut lil-Islaam”. Ndani yake ametaja namna ambavyo anapinga miujiza mingi ya Mtume. Anakereka na miujiza ya Mtume. Kwa kuwa wanakamung hawaamini miujiza ya Mtume. Watu hawa ni katika vifaranga vya wanakanamungu.

Kuhusu ´Abdullaah Daraaz, simjui ni nani.

Kuhusu Abuz-Zahrah, ni mwanafunzi wa Jamaal-ud-Diyn al-Afghaaniy na katika masomo ya Muhammad ´Abduh.

Kuhusu al-Ghazaaliy, himdi zote ni za Allaah kuona Ahl-us-Sunnah wamemuunguza. Allaah ameshamfisha.

Jihaad imewekwa kwa ajili ya kujitetea au pia kwa ajili ya kuvamia? al-Qardhwaawiy anasema kuwa imewekwa kwa lengo la kujitetea peke yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ جَاهِدِ الْكُفَّارَ وَالْمُنَافِقِينَ وَاغْلُظْ عَلَيْهِمْ ۚ وَمَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ

“Ee Nabii! Pambana Jihaad na makafiri na wanafiki na kuwa mgumu kwao; na makazi yao ni Motoni – na ubaya ulioje mahali pa kuishia.” 09:73

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ لِلَّـهِ ۖ فَإِنِ انتَهَوْا فَلَا عُدْوَانَ إِلَّا عَلَى الظَّالِمِينَ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina [shirki] na ´ibaadah zote afanyiwe Allaah pekee, wakikoma basi kusiweko na uadui ila kwa madhalimu.” 02:193

Maneno haya ni batili. Jihaad imewekwa kwa ajili watu waingie katika Uislamu au watoe kodi.

Vita vyote vilivyofanywa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah na Taabi´uun lengo ilikuwa ni hili.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: skaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 47-48
  • Imechapishwa: 08/10/2016