al-Qaradhwaawiy kuhusu ushindi wa Netanyahu

Masiku haya ndugu Swaalih al-Bakriy amenieleza namna alivyomsikia Yuusuf al-Qardhwaawiy akisema:

”Kabla ya kuacha sehemu hii, nataka kusema neno kuhusu matukio ya uchaguzi wa Israel. Waarabu walikuwa wameweka matumaini yao yote kwa ushindi wa Barleen, hata hivyo Barleen imeshindwa. Hata hivyo tunaisifu Israel. Tunatamani lau nchi yetu ingekuwa kama nchi hii. Kwa ajili ya mjumuiko mdogo wa watu wenyewe ndio unahukumu. Hakuna asilimia 94% au asilimia 95% inayoshinda tofauti na tunavyojua katika miji yetu, asilimia 99% kwa asilimia 100%! Mambo gani haya? Lau hata Allaah Mwenyewe angehudhuria kwa watu asingelipata kiasi chote hiki cha kura kutoka kwa watu… Huu ni uongo, udanganyifu na hadaa. Tunaisifu Israel kwa ilichofanya.”

Maneno haya ni upotevu wa wazi. Ikiwa anakusudia kuwafadhilisha mayahudi juu ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ni kafiri. Ikiwa anakusudia kwamba mayahudi, manaswara, mabudha, waabudu wa ng´ombe, waabudu wa tupu na wengine hawatompigia kura Allaah, hili ni khatari kidogo lakini hata hivyo ni upotevu wa wazi.

Allaah (´Azza wa Jall), Mola wetu, hahitajii kura. Hakika Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mwenye kukiambia kitu ”Kuwa!” na kinakuwa. Yeye ndiye ambaye alimwangamiza Fir´awn. Yeye ndiye ambaye alimwangamiza Qaaruun. Yeye ndiye ambaye aliziangamiza nyumati kubwa katika wale waliovuka mipaka na wakaenda kinyume na Mitume wa Allaah (´Azza wa Jall) na akawapa Mitume Wake ushindi duniani na Aakhirah.

Kura hazihitajii mwengine isipokuwa yule mwanaadamu ambaye ni dhaifu. Hata wale wakubwa wa makabila wanakuwa ni wenye kupapatika wakati wa uchaguzi. Kuhusu Mola wetu Yeye hamuhitajii yeyote wala chochote:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ أَنتُمُ الْفُقَرَاءُ إِلَى اللَّـهِ ۖ وَاللَّـهُ هُوَ الْغَنِيُّ الْحَمِيدُ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ بِعَزِيزٍ

”Enyi watu! Nyinyi ni mafakiri kwa Allaah na Allaah ndiye Mkwasi na Mwenye kustahiki kuhimidiwa. Akitaka atakuondosheni mbali na alete viumbe vipya [badala yenu]; na hayo kwa Allaah si yenye kushindikana. 35:15-17

al-Qardhwaawiy! Umekufuru au umemkurubia Allaah? al-Qardhwaawiy huyu anasema kuwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ni Mujaahid, mpambanaji. Mpambanaji? Mpambanaji wa kueneza utata dhidi ya Uislamu.

Isitoshe anawapongeza Israel kwa uchaguzi wa uadilifu. Uchaguzi ni Twaaghuut. Ni mambo yametujia kutoka kwa maadui wa Kiislamu. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَمَا اخْتَلَفْتُمْ فِيهِ مِن شَيْءٍ فَحُكْمُهُ إِلَى اللَّـهِ

”Na katika lolote lile mlilokhitilafiana, basi hukumu yake ni kwa Allaah.” 42:10

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi mlioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wale wenye madaraka katika nyinyi. Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni njia bora na matokeo mazuri zaidi.” (04:59)

Kwa idhini ya Allaah kutatoka kitabu kwa kichwa cha khabari:

”Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy” [Kumnyamazisha mbwa mwenye kubweka Yuusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy]

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waad´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Iskaat-ul-Kalb al-´Aawiy Yusuf bin ´Abdillaah al-Qardhwaawiy, uk. 7-8
  • Imechapishwa: 08/10/2016