al-Kahf baada ya ´Aswr siku ya alkhamisi

Swali: Je, inasihi kusoma Suurah “al-Kahf” baada ya swalah ya ´Aswr siku ya alkhamisi ili mtu aweze kufikia zile fadhilah zilizopokelewa[1]?

Jibu: Kuanzia magharibi ya siku ya alkhamisi.

[1] Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule atakayesoma Suurah “al-Kahf” siku ya ijumaa, basi Allaah atamwangazia nuru kati ya ijumaa mbili.” (Muslim (29/780)).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 35-36
  • Imechapishwa: 01/07/2022