al-Fawzaan kuhusu utumiaji wa hina kwa wanaume

Swali: Ni ipi hukumu kwa wanaume kutumia hina?

Jibu: Ikiwa ni kwa njia ya dawa, hakuna neno. Mwanaume aitumie kwa ajili ya dawa. Ama ikiwa ni kwa ajili ya kujipamba na kujipodoa, hili kuna kujifananisha na wanawake.

Lakini kuna miji ambayo wanaume wanajipamba kwa hina. Hii ni katika ada yao. Ama katika mji wetu sio miongoni mwa ada za wanaume. Miji ambayo sio katika ada zao kujipamba kwa hina haijuzu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (52) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-06-05.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014