al-Fawzaan kuhusu ujinga ni udhuru 5


Swali: Je, mtu anapewa udhuru kwa ujinga katika masuala yote yanayohusiana na ´Aqiydah au kuna masuala ya ´Aqiydah ambayo mtu hapewi udhuru kwayo kwa kutoyajua? Tunaomba utubainishie kidhibiti katika mlango huu.

Jibu: Ujinga umegawanyika sehemu mbili:

1- Ujinga ambao mtu anapewa udhuru kwao.

2- Ujinga ambao mtu hapewi udhuru kwao.

Ujinga aina ya kwanza ambao mtu hapewi udhuru kwao ni yale mambo ya dhahiri kwa mfano wa shirki, kufuru, uchawi, kuua mtu pasi na haki, ribaa, zinaa na kadhalika. Haya ni mambo yako wazi. Yule mwenye kuyakanusha anakufuru. Haya yako wazi katika Qur-aan na Sunnah.
Kuhusiana na mambo yaliyofichikana ambayo hayajui mtu isipokuwa msomi, haya mtu anapewa udhuru kwa ujinga mpaka pale atapowauliza wanachuoni na wakambainishia nayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 28/04/2018