Swali: Ni nani anayeswaliwa Swalah ya ghaibu?

Jibu: Hili lina kauli tatu:

1- Kauli ya kwanza inasema inaswaliwa mtu aliye ghaibu.

2- Kauli ya pili kuko ambao wanasema anaswaliwa ghaibu ikiwa kama hakuswaliwa katika mji wake. Kama mfano wa Najaashiy.

3- Kauli ya tatu kuko ambao wanasema anaswaliwa ikiwa kama ana hadhi katika Uislamu. Kama mfano wa mwanachuoni, mtawala wa Waislamu na mfano wa Najaashiy. Ama Muislamu wa kawaida, huyu inatosheleza kwa wale waliomswalia sehemu yake. Hii ndio kauli sahihi na ndio kauli ambayo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah ameipa nguvu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (70) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13905
  • Imechapishwa: 16/11/2014