Swali 118: Je, wewe umependekeza kitabu kwa anwani “al-Irshaad ilaa Bayaan-il-Haqq fiy Hukm-il-Jihaad”? Je, unapendekeza wasome kitabu hiki cha muheshimiwa Shaykh Ahmad an-Najmiy?

Jibu: Ndio. Kitabu kinawaraddi baadhi ya wale wanaojinasibisha na elimu ambao wamesema kwamba ni lazima kwa watu kwenda Jihaad na wafanye Jihaad hata kama wazazi wao hawako radhi. Ndipo Shaykh Ahmad akamraddi mtu huyo na akabainisha makosa yake katika masuala haya. Kwa hivyo ni kitabu kizuri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 305
  • Imechapishwa: 26/10/2019