Swali: Kuna kidhibiti kipi inapokuja katika kunukuu kutoka katika vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah? Tunaona namna ambavyo Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na Ibn-ul-Qayyim (Rahimahumaa Allaah) wanavyonukuu kwa baadhi ya Ahl-ul-Bid´ah kama al-Ghazaaliy na wengineo.

Jibu: al-Ghazaaliy sio katika Ahl-ul-Bid´ah. Isitoshe kunukuu kutoka kwa Ahl-ul-Bid´ah haijuzu. Kwa sababu wanaweza kumsemea uongo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanaovuliwa tu ni Khawaarij. Wanachuoni wanasema kuwa inafaa kusimulia kutoka kwa Khawaarij kwa sababu wanaharamisha uongo bali wanafikia mpaka kumkufurisha mwenye kusema uongo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (37) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%201%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017