Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika shaytwaan anakimbia kwenye nyumba ambayo kunasomwa ndani yake Suurah “al-Baqarah”.”
Kunakusudiwa Suurah nzima ya “al-Baqarah” au mtu anaweza kusoma kile anachoweza?
Jibu: Ni Suurah nzima, na si kusoma baadhi yake tu. Amesema:
“… kunasomwa ndani yake Suurah “al-Baqarah”.”
Bi maana yote.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (55) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/16503
- Imechapishwa: 23/09/2017