al-Albaaniy mwanamke kusoma Qur-aan bila ya mtandio

Swali: Inajuzu kwa mwanamke kusoma Qur-aan bila ya mtandio?

Jibu: Ndio, inajuzu. Kusoma Qur-aan ni moja katika matendo mazuri na matukufu. Shari´ah haikuweka masharti wala vidhibiti vyovyote. Bali amesema wakati alipokuwa akiwasifu waja Wake wema  na wachaji:

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ

“Wale wanaomdhukuru Allaah hali ya kusimama na hali ya kukaa na kwa kulala ubavuni mwao.”

Kujengea juu ya Aayah hii inafaa kwa yule mwenye kulala ubavu kumdhukuru Mola wake na ukumbusho bora kabisa ni Qur-aan kwa vile ni maneno ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Kwa hivyo inajuzu. Hata hivyo lililo bora ni mtu kusoma akiwa na twahara na katika hali nzuri. Hatuwalazimishi watu jambo hilo, lakini tunawabainishia kuwa ndio jambo kamilifu na bora zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda ”As-ilat-un-Nisaa’”
  • Imechapishwa: 15/03/2019