al-Albaaniy kuhusu manhaj ya Sayyid Qutwub


Ingawa Da´wah ya al-Ikhwaan al-Muslimuun imenufaisha vijana kwa kiwango fulani, Da´wah yao haikujengeka juu ya manhaj ya Salaf. Manhaj hii iliwaasisia Hasan al-Bannaa pamoja na Sayyid Qutwub pia.

Hata hivyo, nafikiria ya kwamba Sayyid Qutwub alibadilika mwisho wa uhai wake wakati alipokuwa ametiwa jela alifanya mabadiliko makubwa kuhusiana na baadhi ya kanuni za Salafiyyah. Hii licha ya kwamba vitabu vyake vya zamani vina makosa mengi bila kujali ikiwa inahusiana na ´Aqiydah au hukumu. Gerezani ilibainika ya kuwa halinganii tena katika ajira hii ambayo haikujengeka juu ya msingi wa Uislamu safi na vitengo visivyoruhusu na kufundisha Uislamu sahihi. Haya ameyaandika katika makala yake maarufu “Limaadhaa a’damuuniy?’ Ninawashauri al-Ikhwaan al-Muslimuun wasome makala hii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alalbany.net/fatawa_view.php?id=6720
  • Imechapishwa: 05/09/2020