al-Albaaniy kuhusu mahali pa mikono baada ya Rukuu´

Baadhi ya ndugu zetu Saudi Arabia na kwenginepo wanatumia hoja kwa Hadiyth hii[1] ya kwamba ni jambo limewekwa katika Shari´ah kuweka/kurudisha mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto katika kisimamo hichi. Ni jambo liko mbali kabisa kutokana na ujumla wa mkusanyiko wa mapokezi na matamshi ya Hadiyth hii kuhusiana na mtu yule aliyekuwa anaswali vibaya. Bali ni jambo batili. Hadiyth kwa mapokezi na matamshi yake mbalimbali haizungumzii kabisa kuweka/kurudisha mikono katika kisimamo hichi. Ni vipi itafaa kuitumia ili kuthibitisha kuwa mkono wa kulia unatakiwa kuwekwa/kurudishwa juu ya mkono wa kushoto baada ya Rukuu´? Hapa ni pale ambapo hayo matamshi yote yatachangia maoni katika hilo. Mtu asemeje ilihali kwa uwazi kabisa zinathibitisha kinyume chake?

Isitoshe uwekaji uliyotajwa mara ya kwanza sio ambao unafahamika kunapotajwa Hadiyht. Mifupa inayokusudiwa katika Hadiyth iliyotajwa ni uti wa mgongo, linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Pindi alipokuwa akiinua kichwa chache anasimama na kunyooka sawasawa mpaka kila pingili ya uti imerudi mahala pake.”

Zingatia na kuwa mwenye inswafu.

Mimi binafsi sina shaka ya kwamba kuweka/kurudisha mikono juu ya kifua katika kisimamo hichi ni Bid´ah inayopotoa. Kwa kuwa kitendo hicho hakikuthibiti kabisa katika Hadiyth zinazohusiana na hukumu za swalah pamoja na wingi wake. Lau kingelikuwa na msingi basi kingelitufikia japo kwa njia moja. Kutokana na ninavyojua hakuna yeyote katika Salaf aliyefanya hivo na wala hakuna imamu yeyote katika maimamu wa Hadiyth aliyelitaja.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Unapoinuka unyooshe mgongo wako na kiinue kichwa chako mpaka mifupa irudi mahala pake.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 120-121
  • Imechapishwa: 10/01/2020