al-Albaaniy hii leo mtu kusema “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsikia mtu akisema katika Tashahhud:

اللهم!إني أسألك بأنَّ لك الحمد، لا اله الا أنت، وحدك لا شَريكَ لَكَ ، المنّان، يا بَديعَ السماوات و الأرض!يا ذا الجلال و الإكرام!يا حي يا قيوم!إِني أَسْأَلُك الْجَنَّة وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa sababu himdi zote ni Zako. Hapana mungu wa haki isipokuwa Wewe, hali ya kuwa upekee huna mshirika. Mwingi wa kuneemesha! Ee mwanzilishi wa mbingu na ardhi! Ee Mwenye utukufu na ukarimu! Ee Uliye hai na Mwenye kusimama kwa dhati Yako! Hakika mimi nakuomba Pepo na najilinda Kwako kutokamana na Moto.”

akasema kuwaambia Maswahabah wake:

“Mnajua alichoomba?” Wakasema: “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema: “Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake amemuomba Allaah kwa jina Lake tukufu. Akiombwa kwalo, Anaitika, na akiulizwa kwalo, Anatoa.”

Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amesema katika maelezo ya chini:

Imezoeleka kwa watu wengi pindi mmoja wao anapoulizwa juu ya kitu asichokijua – ni mamoja kitu hicho kimazowea watu hukijua au kinyume na hivo – wanajibu:

“Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.”

Huku ni kuwa na ujinga juu ya Shari´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa anajua mambo yaliyofichikana wakati wa uhai wake. Kama alivyoelezea Allaah (Ta´ala) katika Qur-aan juu yake:

وَلَوْ كُنتُ أَعْلَمُ الْغَيْبَ لَاسْتَكْثَرْتُ مِنَ الْخَيْرِ وَمَا مَسَّنِيَ السُّوءُ

“Lau ningekuwa najua yaliyofichikana, bila shaka ningelijikithirishia ya kheri na wala nisingepatwa na ovu.” (07:188)

Ni vipi basi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) atajua baada ya kufa? Maoni ya sawa hii leo mtu atosheke kusema:

“Allaah ndiye anajua zaidi.”

Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) walikuwa wakimwambia hivo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ya kujua kwao kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwauliza isipokuwa anajua kitu hicho. Lengo ilikuwa kutaka kuwazindua. Kwa hivyo zinduka juu ya hili na wala usiwe miongoni mwa walioghafilika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Aswl swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 1019
  • Imechapishwa: 01/01/2019