al-Albaaniy Hajuzishi Kuingia Bungeni


Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh: Wewe – Allaah akuhifadhi – umesema kuwa “hushauri” kuingia bungeni. Hiyo ina maana kuwa unajuzisha?

Imaam al-Albaaniy: Hapana. Mimi sijuzishi. Dini ni kupeana nasaha. Hakuna mgongano katika hayo. Mimi simjuzishii muislamu hilo. Ninaposema kuwa simshauri mtu ni kwamba siwezi kumlazimisha mtu mtazamo wangu. Huu ni usulubu wangu katika kuongea. Siwezi kumlazimisha mtu kitu, lakini naweza kumpa maoni yangu na nasaha yangu. Lau watu wangelitaka kunipigia kura mimi, basi nisingeliweza kujiingiza huko maadamu Allaah ananilinda na kunihifadhi. Yanatosheleza maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kwenda kwa mtawala, amewekwa katika mtihani.”[1]

Hii ni katika milango ya mtawala ilio na mitihani mingi. Mimi sijuzishi kabisa kwa muislamu kuingia katika bunge. Lakini huenda akawepo mtu akaniuliza dalili ya kuyaepuka maneno yangu. Wanataka iwe imetajwa katika Qur-aan na Sunnah:

“Haijuzu kuingia katika bunge.”

Elimu yote haiko kwa uwazi kama huo. Kuna kitu kinachoitwa “Ijtihaad” na “Instinbaatw”:

لَعَلِمَهُ الَّذِينَ يَسْتَنبِطُونَهُ مِنْهُمْ

“… wangelijua wale [wenye kujishughulisha na] kutafiti wakabainisha miongoni mwao… “ (04:83)

Hicho ndicho namaanisha.

[1] an-Nasaa’iy (4320). Swahiyh kwa mujibu wa Imaam al-Albaaniy katika ”Swahiyh al-Jaami´ as-Swaghiyr” (6296).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1003)
  • Imechapishwa: 29/01/2017