Aina nyingine ya Irjaa´


Swali: Je, yule asiyemkufurisha mwenye kuacha Swalah kwa ajili ya uvivu anakuwa ni katika Murji-ah?

Jibu: Ndio, hii ni aina ya Irjaa´. Hii ni aina ya Irjaa´. Ikiwa anaamini kuwa matendo sio katika imani ikiwa ni pamoja na Swalah, huyu ni Murji-ah. Ama ikiwa anaamini kuwa matendo ni katika imani lakini akasema kuwa mwenye kuacha Swalah hakufuru, bali ni kama matendo mengine yote yanayopunguza imani na hakufuru, huyu amechukua kauli ya baadhi ya wanachuoni. Wana utata. Pamoja na hivyo hawazingatiwi kuwa ni Murji-ah. Ikiwa anategemea kauli [ya mwanachuoni fulani] na utata anaotumia kama dalili, hakusemwi kuwa ni Mujir-ah. Kunasemwa kuwa amekosea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_08.mp3
  • Imechapishwa: 22/06/2018