Swali: Anayekufa kwa kutetea nchi yake anazingatiwa kuwa ni shahidi? Je, anaswaliwa swalah ya jeneza?

Jibu: Mnajua kuwa Jihaad imegawanyika sehemu mbili:

1 – Jihaad ya kushambulia.

2 – Jihaad ya kujihami.

Jihaad ya kujihami inakuwa pale ambapo adui anavamia mji, basi hapo itakuwa ni wajibu kwa kila yule anayeweza kupigana Jihaad kutetea mji wake na heshima ya Waislamu. Anakuwa anapigana Jihaad katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Katika hali hii akiuawa anakuwa ni shahidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (10) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-29.mp3
  • Imechapishwa: 11/11/2014