Ahl-us-Sunnah wametofautiana kuomba kwa dhati, haki na jahi ya Mtume?

Swali: Kuna wanaosema mtu kusema:

“Ee Mola Wangu! Nakuomba kwa dhati, haki au jaha ya fulani.”

na mfano wa matamko kama haya ni jambo Ahl-us-Sunnah wametofautiana kwalo. Ametumia kisa cha al-´Utbiy na amenukuu hayo kutoka kwa Ibn Qudaamah na Imaam Ahmad katika upokezi mmoja. Je, maneno haya ni sahihi? Je, tofauti hii ni yenye kuzingatiwa?

Jibu: Ndugu! Nimeshawaambia mara nyingi ya kwamba maoni hayazingatiwi midhali hayana dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Kisa cha al-´Utbiy ni batili kutokana na sanadi zake. Zote ni batili na hazikuthibiti. Kisa hiki hakikuthibiti kwa sanadi ambazo ni Swahiyh. Haijalishi kitu hata kama Ibn Kathiyr amekitaja kwenye Tafsiyr yake. Hakukitaja kwa njia ya kwamba anakubaliana nacho. Bali amekisimulia tu. Vilevile mwandishi wa “al-Mughniy” amekitaja kwenye kitabu chake. Kitendo cha kukitaja tu haitoshi kuwa ni dalili. Isitoshe jengine ni kuwa haya ni matendo ya wanaadamu ambao mara wanapatia na mara wanakosea. Haikubaliki kule kimetajwa katika “al-Mughniy” au katika Tafsiyr ya Ibn Kathiyr. Mtu asidanganyike na hilo. Hata kama huyu na yule watasema. Haifai kwa mtu akadanganyika na hilo mpaka kupatikane dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah. Lau tutaenda kwa mtindo huu basi haki itafichikana na batili ndio itadhihiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (11) http://alfawzan.af.org.sa/node/2054
  • Imechapishwa: 14/02/2017