Watu wajinga na waongo kabisa

Raafidhwah ndio watu waliopotea zaidi. Kumepokelewa ima dalili za nukuu au dalili za kiakili na watu hawa ndio watu waliopotea zaidi katika yale yaliyonukuliwa na mambo ya kiakili inapokuja katika madhehebu na mambo yaliyothibitishwa. Hawa hawa wanafanana na wale ambao Allaah amesema juu yao:

وَقَالُوا لَوْ كُنَّا نَسْمَعُ أَوْ نَعْقِلُ مَا كُنَّا فِي أَصْحَابِ السَّعِيرِ

“Watasema: “Lau tungelikuwa tunasikiliza au tunatia akilini, basi tusingelikuwa katika watu wa Motoni.”[1]

Watu hawa ni miongoni mwa watu waongo zaidi katika mapokezi na pia ni miongoni mwa watu wajinga zaidi katika mambo ya kutumia akili. Wanasadikisha mapokezi ambayo wanachuoni wote wanajua kuwa ni ya uongo na wanakadhibisha vitu na mambo ambayo kila mtu anajua kuwa ni ya kweli na ambayo pia yamepokelewa kwa njia nyingi kizazi baada ya kizazi.

Inapokuja katika wanaume walioko katika cheni ya wapokezi, hawawezi kupambanua kati ya wale waliotambulika kwa uongo, makosa au ujinga na kati ya wale wenye kutambulika kwa uadilifu, kuhifadhi, kuyadhibiti mambo na utambuzi juu ya mapokezi.

Wanachotegemea ni kufuata kichwa mchunga ilihali wao wenyewe wanaona kuwa wamesimamisha dalili. Mara utawaona wanawafuata Mu´tazilah na Qadariyyah na mara utawaona wanawafuata Mujassimah na wakati mwingine utawaona wanawafuata Jabriyyah na wao [Raafidhwah] ndio wajinga kabisa katika mapote yote haya inapokuja katika mambo ya kinadharia. Kwa ajili hiyo wanachuoni ni wenye kuwaonelea kuwa miongoni mwa wajinga kabisa kati ya waislamu.

[1] 67:10

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/8-9)
  • Imechapishwa: 03/02/2019