Afupishe au akamilishe msafiri aliyefika katika mji wake na hajaswali?


Swali: Wakati wa swalah ukimkuta mtu katika hali ya safari akielekea katika mji wake na asiswali swalah hiyo isipokuwa baada ya kufika katika mji wake – aiswali kikamilifu au kwa kufupisha?

Jibu: Aiswali kikamilifu. Kama nimeelewa vyema ni kwamba mtu anaelekea katika mji wake na wakati ukamwingilia, je, atapofika katika mji wake aswali kikamilifu au kwa kufupisha? Jibu tunasema aswali kwa kukamilisha. Kama ambavyo kinyume chake anatakiwa kuswali kwa kufupisha. Kwa msemo mwingine ni kwamba endapo muadhini ataadhini na wewe uko katika mji wako kisha ukasafiri kabla ya kuswali, je, unatakiwa kuswali Rak´ah nne au mbili? Maoni yaliyo na nguvu ni kwamba unatakiwa kuswali Rak´ah mbili. Kinachozingatiwa ni kile kitendo cha kuswali. Kwa hivyo inasemwa iwapo mtu atapofika katika mji wake kabla hajaswali na wakati umeshamwingilia, basi anatakiwa kuswali Rak´ah nne. Vivyo akitoka katika mji wake akiwa ni msafiri na akawa hajaswali, basi anatakiwa kuswali Rak´ah mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37)
  • Imechapishwa: 19/04/2018