Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

17- Abu Ya’laa Shaddaad bin ´Aws (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika Allaah ameamrisha kufanya wema katika kila kitu. Kwa hiyo unapoua, ua kwa uzuri na unapochinja chinja kwa uzuri. Basi kila mmoja wenu anoe kisu chake barabara na amuondoshee machungu [asimtese] yule mnyama anayemchinja.”

Hii ni dalili ya [maamrisho ya] kutumia kifaa kizuri [chenye makali] wakati wa kutaka kutoa roho kwenye wanyama. Ni kitu kinachoenda kinyume na wema yale yanayofanywa na baadhi ya watu, nayo ni kuwa hajui kuchinja na anataka kwenda kujifunza namna ya kuchinja. Anarefusha muda kwa dakika kama kumi, dakika tano na huku yuko anaichinja na akaichinja kimakosa. Mambo kama haya yanakwenda kinyume na maamrisho ya kufanya wema wakati wa kuua au wakati wa kuchinja. Kinachotakiwa ni mtu awachinje wanyama kwa haraka. Kisu kiwe na makali na awe ni mjuzi wa kuchinja. Huu ni wema tuliyoamrishwa.

Hata miongoni mwa wema ambao tumeamrishwa kufanya imepokelewa ya kwamba mtu asichinje mnyama mbele ya mnyama mwingine ili asiudhike kwa kuona damu za ndugu yake pindi anapochinjwa.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 262
  • Imechapishwa: 22/05/2020