Ada iliyoenea katika miji mingi ya waislamu kuogopa kula vichinjwa vya Ahl-ul-Kitaab

Swali: Katika nchi yetu kuna desturi, kama kwa makafiri pia, watu hawali kichinjwa isipokuwa kilichochinjwa na muislamu. Mtu huyu muislamu anachukua kutoka kwao kiwango fulani cha pesa. Je, kitendo hichi kinafaa?

Jibu: Kitu cha kwanza kitendo chao kwamba hawali isipokuwa tu anapochinja muislamu ni kosa. Kwa sababu Allaah ametuhalalishia vile vinavyochinjwa na mayahudi na wakristo. Amesema (Ta´ala):

وَطَعَامُ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ حِلٌّ لَّكُمْ وَطَعَامُكُمْ حِلٌّ لَّهُمْ

“… na chakula cha wale Ahl-ul-Kitaab ni halali kwenu.”[1]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Chakula.”

Bi maana vichinjwa vyao.

Kuna watu aina tatu ambao ni halali vichinjwa vyao:

1- Muislamu.

2- Myahudi.

3- Mkristo.

Muislamu akichinja kichinjwa na akaomba malipo juu yake, ni mamoja kabla au baada ya kuchinja, hakuna ubaya. Kwa sababu hii ni kazi ya halali. Kuchukua malipo juu ya kazi ya halali ni jambo la halali.

[1] 05:05

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (94) http://binothaimeen.net/content/3875
  • Imechapishwa: 15/01/2020