Swali: Je, inafaa kuandika baadhi ya Aayah za Qur-aan tukufu, kama mfano wa Aayah ya Kursiy, katika vyombo vya chakula kwa lengo la kujitibu kwazo?

Jibu: Tunapasa kujua kuwa Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall) ni kitukufu na kimetakasika zaidi kutokamana na kukitweza na kukidhalilisha katika kiwango hichi. Ni vipi nafsi ya muumini itahisi utulivu kuiweka Aayah tukufu zaidi ya Qur-aan ndani ya chombo ambamo itatwezwa, kutupwa na watoto kucheza nayo? Hapana shaka kwamba kitendo hichi ni haramu. Ni lazima kwa yule anayefanya kitu kama hicho ni kuzifuta Aayah hizo ndani yake. Ikishindikana kufanya hivo basi azizike maeneo ambapo ni pasafi. Ama kubaki nazo, akazidhalilisha ambapo watoto wakanywa kutoka humo na wakacheza nazo basi anapaswa kutambua kuwa Salaf hawakujibu kwa Qur-aan kwa njia kama hiyo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/68-69)
  • Imechapishwa: 12/08/2021