99. Sura ya tatu: Mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah juu ya kuwaraddi wazushi

Mfumo wao katika jambo hilo umejengwa juu ya Qur-aan na Sunnah. Ni mfumo wenye kukinaisha na imara. Kwani wanaziraddi shubuha za wazushi na kuzivunjavunja na wanatumia dalili za Qur-aan na Sunnah juu ya ulazima wa kushikamana barabara na Sunnah na kukataza Bid´ah na mambo yaliyozuliwa. Wametunga vitabu vingi juu ya hilo na wakawaraddi Shiy´ah, Khawaarij, Jahmiyyah, Mu´tazilah na Ashaa´irah katika vitabu vya ´Aqiydah juu ya mirengo yao iliyozuliwa katika misingi ya imani na misingi ya ´Aqiydah. Vilevile wametunga vitabu maalum juu ya jambo hilo. Ni kama ambavo Imaam Ahmad alivyotunga kitabu “ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” na maimamu wengine wakatunga katika jambo hilo. Kama mfano wa ´Uthmaan bin Sa´iyd ad-Daarimiy, kama ilivyo kwenye vitabu vya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn-ul-Qayyim, Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wengineo ambao wameraddi mapote hayo, waabudia makaburi na Suufiyyah.

Kuhusu vitabu maalum vinavyowaraddi Ahl-ul-Bid´ah ni vingi. Miongoni mwa vitabu vya kale kwa njia ya mfano ni vifuatavyo:

1- “al-I´tiswaam” cha Imaam ash-Shaatwibiy.

2- “Iqtidhwaa´-us-Swiraatw al-Mustaqiym” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Sehemu yake kubwa imewaraddi wazushi.

3- “Inkaar-ul-Hawaadith wal-Bid´ah” cha Ibn Wadhdhwaah.

4- “al-Hawaadith wal-Bid´ah” cha at-Twartwuushiy.

5- “al-Baa´ith ´alaa Inkaar-il-Bid´ah wal-Hawaadith” Ibn Shaamah.

Miongoni mwa vitabu vya leo:

1- “al-Ibdaa´ fiy madhwaar-il-Ibtidaa´” cha Shaykh ´Aliy Mahfuudhw.

2- “as-Sunan wal-Mubtadi´aat al-Muta´aliqah bil-Adhkaar was-Swalawaat” cha Shaykh Muhammad bin Ahmad ash-Shaqiyriy al-Hawaamidiy.

3- “at-Tahdhiyr minal-Bid´ah” cha Shaykh ´Abdu-´Aziyz bin Baaz.

Himdi zote njema anastahiki Allaah kuona wanachuoni wa waislamu bado mpaka hii leo ni wenye kuendelea kukaripia Bid´ah na wanawaraddi watu wa Bid´ah kupitia magazeti, majarida, redio, Khutbah za ijumaa, nad-wah na mihadhara mambo ambayo yana athari kubwa katika kuwaelewesha waislamu kuzitokomeza Bid´ah na kuwasambaratisha wazushi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 191-192
  • Imechapishwa: 09/07/2020