98. Kukirihishwa kunakuwa katika neno au kitendo na si moyoni

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Aayah inafahamisha namna hii kwa njia mbili:

1 – Ni maneno Yake:

إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ

“… isipokuwa yule aliyekirihishwa na huku moyo wake umetua juu ya imani.” (16:106)

Allaah (Ta´ala) hakumbagua yeyote isipokuwa tu yule aliyelazimishwa, na ni jambo linalojulikana ya kwamba mtu hatenzwi nguvu isipokuwa katika maneno au kitendo. Ama ´Aqiydah [Itikadi] ndani ya moyo, hakuna anayelazimishwa kwayo.

MAELEZO

Allaah (Ta´ala) hakumbagua yeyote katika Aayah isipokuwa tu yule mwenye kulazimishwa. Wengine wote ni makafiri. Kulazimishwa kunakuwa ima kwa neno au kitendo. Kuhusiana na ´Aqiydah ya moyo, hakuna mwengine anayeijua isipokuwa Allaah pekee. Ni jambo lisiloweza kufikiriwa kuwa kuna ambaye anaweza kutenzwa nguvu kwa hilo. Ni jambo lisilowezekana mtu akamlazimisha mwengine kuamini namna fulani. Hili ni jambo lililofichikana na hakuna anayelijua. Kulazimishwa kunakuwa katika yale yanayodhihiri katika neno au kitendo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 104
  • Imechapishwa: 02/12/2023