98. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tisa wa an-Nisaa´


al-´Ayyaashiy amesema:

“Zaraarah amehadithia ya kwamba Abu Ja´far amesema: “Nundu ya juu kabisa ya Uislamu, mlango wa Mitume na radhi za Allaah zinapatikana katika kuwatii maimamu baada ya kumtambua. Allaah amesema:

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا

“Atakayemtii Mtume basi huyo amemtii Allaah; na atakayempa mgongo basi [atambue] hatukukutuma kuwa mlinzi juu yao.”[1]

Lakini ikiwa mtu atasimama nyusiku zake, akafunga michana yake, akatoa swadaqah mali zake zote na akahiji maisha yake yote bila ya kutambua uongozi wa kiongozi wa Allaah, basi hatokuwa na haki ya kupata thawabu za Allaah wala hatokuwa katika waumini.”[2]

Allaah amemtakasa Abu Ja´far kutokamana na uongo huu ambao hauwezi kutoka isipokuwa kutoka kwa Raafidhwah Baatwiniyyah. Lau ingelikuwa ni kweli alisema hivo basi yangelikuwa ni maneno ya batili na uzushi juu ya Allaah ambao atamfanyia hesabu kwao.

Nundu ya juu kabisa ya Uislamu ni Jihaad katika njia ya Allaah, kama alivyosema Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Radhi za Allaah zinapatikana katika kumuamini Yeye, Mtume wake, Vitabu Vyake na Malaika Wake, kumtii Yeye na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kushikamana na Qur-aan na Sunnah.

Kumtambua imamu ambaye amezuliwa na Raafidhwah si sharti yoyote juu ya kusihi kwa imani na wala radhi za Allaah hazikufungamana na chochote katika hayo. Allaah hatowafanyia hesabu watu iwapo watakuwa si wenye kumjua imamu huyu aliyezuliwa.

Yule ambaye atamuamini imamu huyu kwa mujibu wa madhehebu ya Raafidhwah na akampa cheo kilekile walichomzulia basi atakuwa katika Raafidwah wapotevu walioangamia.

[1] 08:80

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/259).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 146
  • Imechapishwa: 02/12/2017