97. Tofauti ya kuacha au kukanusha nguzo na tanzu


Hii ndio tofauti kati ya tanzu na nguzo. Mwenye kuacha kitu katika nguzo basi anakufuru. Anayekanusha Tawhiyd na akamshirikisha Allaah anakufruu. Kwa sababu ameacha nguzo ya kwanza. Mwenye kumpinga mmoja katika Mitume anakufuru. Kwa sababu ameacha nguzo moja wapo miongoni mwa nguzo za Uislamu. Mwenye kuwapinga Malaika anakufuru na kutoka nje ya dini. Mwenye kukufuru kufufuliwa, akakanusha Pepo, Moto, njia, mizani au chochote katika yale yaliyothibiti katika mambo ya Aakhirah basi anakufuru kwa jambo hilo. Kwa sababu amepinga nguzo miongoni mwa nguzo za imani. Vivyo hivyo yule mwenye kupinga Qadar na akasema kuwa mambo yanapitika bila ya ujuzi wa Allaah, kwamba hayakutanguliwa na kukadiriwa na Allaah, kwamba yanatokea bahati nasibu na kwamba hakuna Qadar – kama wanavosema Mu´tazilah waliopindukia – anakufuru. Kwa sababu amekanusha Qadar. Kuhusu yule mwenye kuacha kitu katika tanzu basi imani yake inapungua. Ima ikawa ni kupungua kwa ule ukamilifu wake wa lazima au ni kupungua kwa ukamilifu wake uliyopendekezwa. Lakini hakufuru kwa jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 205
  • Imechapishwa: 24/01/2021