92. Kusimama katika Rak´ah ya tatu na Rak´ah ya nne

Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

الله أكبر

“Allaah ni mkubwa.”

na kusimama katika Rak´ah ya tatu[1]. Alimwamrisha yule mtu aliyeswali vibaya na akasema:

“Kisha ufanye hivo katika kila Rak´ah na Sajdah.”

Alipokuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anainuka kutoka kwenye kitako anasema:

الله أكبر

“Allaah ni mkubwa.”

halafu ndio anasimama[2].

Wakati fulani alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaweza kunyanyua mikono yake[3] pamoja na Takbiyr hii. Alipokuwa anataka kusimama kwenda katika Rak´ah ya nne basi husema:

الله أكبر

“Allaah ni mkubwa.”[4]

Alimwamrisha yule mtu aliyeswali vibaya kufanya vivyo hivyo. Wakati fulani (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akinyanyua mikono yake[5] pamoja na Takbiyr hii.

Kisha akikaa hali ya kulingana juu ya mguu wake wa kushoto barabara mpaka kila mfupa unarudi mahala pake stahiki. Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasimama hali ya kujisaidia juu ya ardhi[6].

Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akikunja ngumi hali ya kutegemea mikono yake anaposimama[7].

Katika kila Rak´ah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisoma “al-Faatihah”. Alimwamrisha kufanya hivo yule mtu aliyeswali kimakosa. Katika zile Rak´ah mbili za mwisho za Dhuhr wakati mwingine (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiongeza baadhi ya Aayah chache. Tayari hilo limekwishatangulia katika mlango unaozungumzia kisomo cha Dhuhr.

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

[2] Abu Ya´laa katika ”al-Musnad” (2/284). Cheni ya wapokezi ni nzuri. Imetajwa katika ”as-Swahiyhah” (604).

[3] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[4] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[5] Abu ´Awaanah na an-Nasaa’iy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[6] al-Bukhaariy na Abu Daawuud.

[7] al-Harbiy katika ”Ghariyb-ul-Hadiyth”. Kadhalika maana kama hiyo imepokelewa na al-Bukhaariy na Abu Daawuud. Ama kuhusu Hadiyth:

“Amekataza (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu kutegemea mikono yake pindi anaposimama katika swalah.”

ni dhaifu sana na haikusihi. Hayo nimeyabainisha katika “adh-Dhwa´iyfah” (967).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 07/01/2019