91. Kumtamkisha maiti shahaadah baada ya kuzikwa


Swali 91: Ni ipi hukumu ya kutamkisha shahaadah baada ya kumaliza kuzika[1]?

Jibu: Ni Bid´ah na ni jambo halina msingi. Haifai kutamkisha shahaadah baada ya kufa. Kumepokelewa juu ya hilo Hadiyth zilizotungwa na ni jambo halina msingi. Kumtamkisha shahaadah maiti kunakuwa kabla ya kufa.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/206).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 64
  • Imechapishwa: 05/01/2022