Swali 09: Baadhi ya vyumba ya wagonjwa vina TV. Wako baadhi ya wagonjwa ambao wametaka hivyo na wengine hawakutaka hivyo kwa sababu zinawasababishia dhiki na tashwishi. Tufanye nini?

Jibu: Katika hali kama hii mgonjwa akiwa kwenye chumba ambacho wapo wagonjwa wengine wasiotaka TV, basi asiwawashie TV. Yote haya ni kwa ajili ya kuzikusanya nyoyo na kujiepusha na fitina. Na kama wote wataitaka basi hakuna kizuizi muda wa kuwa wanachotazama ni mambo yanayowanufaisha, kama vile Qur-aan, kujifunza elimu na mengineyo yanayowanufaisha katika dini na dunia yao. Lakini wafanye hivo kwa kuweka sauti ya chini. Wasitazame mambo yenye kuwadhuru kama vile nyimbo, pumbao na mfano wake. Wakikiondosha kabisa basi hilo ndilo salama na zuri zaidi. Hakika wao wanajua zaidi ni kipi chenye manufaa zaidi juu ya nafsi zao. Ama kuwalazimisha [wagonwa wengine] kitu chenye kuwadhuru na kuwaudhi na huenda kikawakosesha usingizi na kupumzika na pengine baadhi ya wapumbavu hawawajali nduug zao wagonjwa, kitendo hicho hakijuzu.

Lililo la wajibu chini ya shingo la mtu awe na uaminifu ambao kwao anamcha Allaah juu yao kwa njia ya kwamba asishughulishwe isipokuwa na kitu kinachowanufaisha na kuwaridhisha. Vinginevyo akifunge kama hawapendi jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 30-31
  • Imechapishwa: 18/05/2019