9. Safari ya Mtume kwenda at-Twaaif


Wakati ilani ilipoondoka Khadiyjah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na Abu Twaalib wote wakafariki. Walipishana kwa siku tatu. Kwa hivyo watu wa mji wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakamzidishia matatizo zaidi na kumshabulia. Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akatoka kwenda at-Twaaif ili raia wa mji wamhifadhi, kumnusuru dhidi ya watu wa mji wake na kumlinda nao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawalingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall), hawakumuitikia kitu katika aliyowalingania. Badala yake wakamuudhi maudhi makubwa kabisa. Watu wa mji wake hawakuwahi kumuudhi sana kama jinsi walivyomuuadhi. Hivyo basi akarejea kutoka kwao na akarudi Makkah tena chini ya ulinzi wa al-Mutw´im bin ´Adiyy bin Nawfal bin ´Abdi Manaaf.

Akaanza kuwalingania katika dini ya Allaah (´Azza wa Jall) ambapo at-Twufayl bin ´Amr ad-Dawsiy akaingia katika Uislamu. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuomba Allaah amjaalie afanye miujiza ambapo Allaah akafanya katika uso wake akawa na nuru. Akasema:

“Ee Mtume wa Allaah! Ninachelea wakaja kusema kuwa huku ni kuumbuka.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamuomba tena na akapata nuru kwenye sauti yake. Hivyo akawa ni mwenye kujulikana kama mtu mwenye nuru.

at-Twufayl pia akawalingania watu wake katika dini ya Allaah na baadhi yao wakaingia katika Uislamu. Akabaki katika mji wake. Wakati Allaah alipomfanya Mtume Wake kuiteka Khaybar akafika huko na zaidi ya familia thamanini.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 26
  • Imechapishwa: 18/03/2017