89. al-Qummiy upotoshaji wake wa sita wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

فَمِنْهُم مَّنْ آمَنَ بِهِ وَمِنْهُم مَّن صَدَّ عَنْهُ ۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا

“Miongoni mwao wako waliomuamini na miongoni mwao wako waliomkengeuka. Na Moto uwakao kwa nguvu ni wenye kuwatosha.”[1]

“Bi maana [miongoni mwao wako waliomuamini] kiongozi wa waumini nao ni Salmaan, Abu Dharr, al-Miqdaad na ´Ammaar. Na miongoni mwao wako waliomkengeuka nao ni wale waliowapokonya familia ya Muhammad na wafuasi zao haki zao. Juu yao kumeteremshwa:

وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا

“Na Moto uwakao kwa nguvu ni wenye kuwatosha.”[2]

Madhehebu ya chuki ya Raafidhwah dhidi ya Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yamewaondosha akili kiasi cha kwamba wamesibiwa kuwa waongo wakubwa na watu wenye tabia duni kabisa. Hakuna yeyote anayemsemea Allaah uongo khatari kama wao. Hakuna yeyote anayekipotosha Kitabu cha Allaah kitukufu kama wao.

Aayah zilizotajwa zinawahusu mayahudi na namna walivyomkufuru Mtume wa Allaah Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale aliyokuja nayo pamoja vilevile na jinsi walivyoyakufuru yale aliyokuja nayo Ibraahiym na kizazi chake bora katika Mitume na waumini. Raafidhwah wanazielekeza kwa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kuwalaani, kuwakufurisha na kuwadumisha Motoni milele. Pindi Raafidhwah wanapozungumzia imani wanakusudia kumuamini Allaah na maimamu peke yao. Kwa mujibu wao waumini watu wane tu: Salmaan, Abu Dharr, al-Miqdaad na ´Ammaar.

[1] 04:55

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/140-141).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 131-132
  • Imechapishwa: 20/11/2017