85. Mitume wote wametumwa kwa kazi moja


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah ameutumia kila Ummah Mtume, kuanzia kwa Nuuh mpaka kwa Muhammad, ili kuwaamrisha kumwabudu Allaah pekee na akiwakataza na shirki. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Na kwa hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na waungu wa wongo!” (an-Nahl 16 : 36)

MAELEZO

Allaah ameutumia kila Ummah Mtume – Allaah ameutumia kila Ummah Mtume akiwaita wamwabudu Allaah pekee na akiwakataza na shirki. Dalili ya hilo ni maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَإِن مِّنْ أُمَّةٍ إِلَّا خَلَا فِيهَا نَذِيرٌ

“Hakuna Ummah wowote ule isipokuwa amepita humo mwonyaji.” (Faatwir 35 : 24)

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

“Na kwa hakika Tulituma katika kila ummah Mtume [awaamrishe watu wake] kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na waungu wa wongo!”

Hii ndio maana ya hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 150
  • Imechapishwa: 04/06/2020