81. Ndio maana waumini watamuona Mola wao siku ya Qiyaamah

Abu Muhammad ´Abdullaah bin Abiy Zayd al-Qayrawaaniy (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Subhaanah) ameiumba Pepo na kuifanya kuwa ni makazi ya milele juu ya vipenzi Vyake.

MAELEZO

Neema kubwa ambayo Allaah atawapa watu wa Pepo ni kutazama uso Wake mtukufu. Kwa vile walimwamini duniani pasi na kumuona basi Allaah atajidhihirisha kwao Peponi ambapo wamuone na macho yao yaburudike kwa kumuona. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika nyinyi mtamuona Mola wenu kama mnavouona mwezi mwandamo – hamtosongamana katika kumuona.”[1]

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Ee Mtume wa Allaah! Je, sisi tutamuona Mola wetu siku ya Qiyaamah?” Mtume wa Allaah akasema: “Je, kwani nyinyi mnasongamana katika kutazama jua mchana kweupee pasipo mawingu?” Wakasema: “Hapana, ee Mtume wa Allaah.” Ndipo akasema: “Basi vivyo hivyo ndivo mtamuona Mola wenu siku ya Qiyaamah.”[2]

Hii ni neema kwa waumini kwa vile walimuamini duniani pasi na kumuona. Walimuamini kwa dalili za kukata zilizofahamishwa na maelezo ya Mitume na Aayah za Qur-aan na alama za ulimwengu juu ya uwepo Wake (Subhaanahu wa Ta´ala). Ndio maana Allaah akawatunuku siku ya Qiyaamah wamuone.

[1] al-Bukhaariy (554) och Muslim (633).

[2] al-Bukhaariy (4581) na Muslim (183).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 18/08/2021