81. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kwanza wa an-Nisaa´


al-´Ayyaashiy amesema pindi alipokuwa akifasiri Aayah:

فَإِنْ آنَسْتُم مِّنْهُمْ رُشْدًا فَادْفَعُوا إِلَيْهِمْ أَمْوَالَهُمْ

“Mkihisi kuwa wamepevuka, basi wapeni mali zao.”[1]

“´Abdullaah bin al-Mughiyrah ameeleza kuwa Ja´far bin Muhammad amesema: “Maana yake ni kwamba mkiona wanaipenda familia ya Muhammad basi zinyanyueni daraja zao.”[2]

Kumpenda Allaah, Malaika Wake, Mtume Wake, Maswahabah na waumini wengine wote ni jambo la wajibu. Familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanaingia katika waumini. Lakini hata hivyo hii sio maana ya Aayah. Ni kwa nini familia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tu ndio ifanywe kuwa mtihani ikiwa inahusiana na kupima imani ya mtu? Upevukaji unaomaanishwa katika Aayah ni kuwa na dini na busara ya kuhifadhi mali, hivyo ndivyo alivyosema Ibn ´Abbaas, wafasiri wa Qur-aan na wanachuoni. Tazama Tafisiyr ya Ibn Kathiyr (03/354).

[1] 04:06

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/221).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 119
  • Imechapishwa: 13/04/2017