79. Je, inafaa kufunua uso wa maiti akilazwa ndani ya mwanandani?


Swali 79: Je, inafaa kufunua uso wa maiti akilazwa ndani ya mwanandani[1]?

Jibu: Haijuzu kufunua uso wa maiti akilazwa katika mwanandani. Ni mamoja atakuwa ni mwanamme au mwanamke. Hakika si venginevyo ni lazima kumsitiri kwa sanda. Isipokuwa akiwa ni Muhrim. Haifai kumfunika kichwa wala uso wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu ya ambaye amekufa hali ya kuwa ni Muhrim:

“Muosheni maiti kwa maji yaliyochanganyikana na mkunazi, mumkafini katika nguo zake na wala msifunike kichwa wala uso wake. Kwani hakika atafufuliwa siku ya Qiyaamah hali ya kuwa ni mwenye kuleta Talbiyah.”[2]

Kuna maafikiano juu yake na tamko ni la Muslim.

Lakini maiti akiwa ni mwanamke uso wake unafunikwa ijapo atakuwa ni Muhrim. Kwa sababu uso wake hautakiwi kuonekana.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/194).

[2] al-Bukhaariy (1851) na Muslim (1206) na tamko ni lake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 01/01/2022