78. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na sita wa Aal ´Imraan


al-´Ayyaashiy amesema:

“´Umar bin ´Abdir-Rahmaan bin Kathiyr amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah aliyesema kuhusiana na maneno Yake:

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ

“Mola wetu! Hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye imani: – ‘Mwaminini Mola wenu!’ – basi tukaamini. Mola wetu! Tusamehe madhambi yetu na utufutie makosa yetu na Tufishe pamoja na waja wema!”[1]

“Ni kiongozi wa waumini aliyeitwa kutoka mbinguni: “Mwamini Mtume!” Basi akawa amemuamini.”[2]

´Aliy peke yake tu ndiye aliyemuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kwani ´Aliy hakumuamini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka aitwe na mwenye kuita kutoka mbinguni? Ni ubaya uliyoje Raafidhwah walivyo! Ni ujasiri uliyoje walionao katika kuisemea Qur-aan uongo na kuipotosha!

Aayah ina maana kwamba waumini walisikia mlinganizi anawalingania katika dini ya Allaah. Mlinganizi huo alikuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); wakamuamini na kumfuata. Raafidhwah wanakengeusha maana ya Allaah na ikawa kama unavyoona mwenyewe:

فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَـٰذَا مِنْ عِندِ اللَّـهِ لِيَشْتَرُوا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ

“Basi ole kwa wale wenye kuandika kitabu kwa mikono yao kisha wakadai kuwa hayo ni kutoka kwa Allaah ili wayabadilishe kwa thamani ndogo! Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao na ole wao kwa yale wanayoyachuma!”[3]

[1] 03:193

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/211).

[3] 02:79

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 116
  • Imechapishwa: 13/04/2017