78- Asome kimyakimya. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Umaamah bin Sahl ambaye amesema:

“Sunnah katika swalah ya jeneza ni mtu asome katika ile Takbiyr ya kwanza mama wa Qur-aan kimyakimya, kisha apige Takbiyr tatu na alete Tasliym katika ile ya mwisho.”

Ameipokea an-Nasaa´iy na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kama ilivyotangulia katika masuala ya 74, Hadiyth ya tano, namba 1, uk. 111.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 154
  • Imechapishwa: 02/02/2022