75. Namna hii yanafutwa madhambi madogomadogo


Madhambi yamegawanyika aina mbili: makubwa na madogo. Dalili ya hilo ni maneno ya Allaah (Ta´ala):

إِن تَجْتَنِبُوا كَبَائِرَ مَا تُنْهَوْنَ عَنْهُ نُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَنُدْخِلْكُم مُّدْخَلًا كَرِيمًا

“Endapo mtajiepusha na madhambi makubwa mnayokatazwa, basi Tutakufutieni madhambi yenu madogo na tutakuingizeni katika mahali patukufu.”?[1]

Madhambi madogo yanafutwa ingawa mwenye nayo hakutubu kwayo; yanafutwa kwa kuepuka madhambi makubwa. Ambaye anayaepuka madhambi makubwa basi anasamehewa kwa madhambi madogo. Madhambi madogo yanasamehewa pia kwa matendo mema. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Lifuatishie ovu jema litaifuta.”[2]

Majanga mbalimbali yanayompata mtu yanafuta madhambi madogo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna muislamu anayefikwa na machovu, tabu, ugonjwa, hamu, huzuni mpaka mwiba ukimchoma, isipokuwa Allaah anamfutia makosa yake.”[3]

Mitihani mbalimbali inafuta makosa ya muislamu. Yako mambo mengine vilevile yanayofuta makosa.

[1] 4:31

[2] at-Tirmidhiy (1987).

[3][3] al-Bukhaariy (5641-5642).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 57-58
  • Imechapishwa: 16/08/2021