Kuulizauliza maswali mengi yasiyokuwa na maana  

Hakika kuuliza maswali mengi ni jambo lisiloonyesha uelewa katika Dini, unyenyekevu wala kutafuta elimu. Inapaswa kwa mtu mwenye kuitaka haki, mtu mwenye Dini na kheri apunguze kuuliza-uliza maswali kiasi na itakavyowezekana. Allaah (Jalla wa ´Alaa) Amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ وَإِن تَسْأَلُوا عَنْهَا حِينَ يُنَزَّلُ الْقُرْآنُ تُبْدَ لَكُمْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهَا

“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyaulizia pale inapoteremshwa Qur-aan mtadhihirishiwa. Allaah Ameyasamehe hayo. ” (05:101)

Kuuliza juu ya jambo ambalo halikuja katika Shari´ah sio katika mfumo wa Ahl-ul-Ittibaa´, bali linalopasa ni kuuliza juu ya jambo lililokuja katika Shari´ah.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 187
  • Imechapishwa: 17/05/2020