b) Baadhi ya wanawake na wasimamizi wao kuchukulia wepesi mwanamke kupanda gari peke yake akiwa na dereva ambaye sio Mahram yake licha ya kuwa kitendo hicho ni faragha iliyoharamishwa. Shaykh Muhammad bin Ibrahiym Aalush-Shaykh (Rahimahu Allaah), ambaye alikuwa Muftiy wa Saudi Arabia, amesema katika “Majmuu´-ul-Fataawaa”:

“Hivi sasa hakukubaki mashaka yoyote juu ya kwamba mwanamke wa kando kupanda gari peke yake na dereva, pasi na Mahram wa kuandamana naye, ni maovu ya wazi. Ndani yake kuna uharibifu ambao haitakiwi kuuchukulia wepesi. Ni mamoja mwanamke huyo ni mtoto mwenye utulivu na anayejichunga na mambo machafu. Mwanaume ambaye anaridhia jambo hili kwa wanawake, Mahram zake ni wenye dini dhaifu, umepungua wanaume wake na mwenye wivu kidogo juu ya Mahram zake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamume hakai faragha na mwanamke isipokuwa shaytwaan huwa ni watatu wao.”

Mwanamke kupanda ndani ya gari na mwanamume ni kukubwa zaidi kuliko faragha ndani ya nyumba na kwenginepo. Kwa sababu anaweza kwenda naye popote anapotaka ndani ya nchi au nje ya nchi, kwa kutaka kwake au pasi na kutaka kwake. Matokeo yake yakapelekea katika uharibifu mkubwa kuliko yale yanayopelekea katika faragha kama faragha.”[1]

Ni lazima mtu ambaye atamwondoshea faragha hiyo awe mkubwa. Haitoshi kuwepo kwa mtoto. Yale wanayofikiria baadhi ya wanawake kwamba wakiandamana na mtoto faragha itakuwa yenye kuondoka ni dhana ya kimakosa. Imaam an-Nawawiy amesema:

“Mwanaume wa kando akikaa faragha na mwanamke wa kando pasi na wawili hao kuwa na mtu wa tatu ni jambo la haramu kwa maafikiano ya wanachuoni. Vivyo hivyo kama watakuwa na mtu ambaye haonelewi haya kwa sababu ya udogo wake haiondoki ile faragha iliyoharamishwa.”[2]

[1] (10/52).

[2] (09/109).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 125-126
  • Imechapishwa: 12/12/2019