72. Hijrah ni kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda wa Kiislamu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hijrah ni kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu.

MAELEZO

Hijrah kilugha maana yake ni “kukiacha kitu”. Ama maana yake katika Shari´ah ni kama alivyosema Shaykh:

“Hijrah ni kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu.”

Mji wa kikafiri ni ule ambao kunatekelezwa ndani yake nembo za kikafiri na hakutekelezwi nembo za Kiislamu kama mfano wa adhaana, swalah za mkusanyiko, sikukuu na ijumaa kwa njia ya jumla na iliyoenea. Tumesema kwa njia ya jumla na iliyoenea ili zitoke zile nembo za Kiislamu zinazofanywa kwa njia iliyofupika katika nchi za kikafiri zilizo na waislamu wachache. Nchi hizi hazizingatiwi kuwa ni za Kiislamu kwa sababu tu ya zile nembo za Kiislamu wanazotekeleza. Ama mji wa Kiislamu ni ule mji ambao kunatekelezwa nembo hizi za Kiislamu kwa njia ya jumla na iliyoenea.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 03/06/2020